Halmashauri ya Wilaya ya Songea ilipokea fedha kiasi cha shilingi Bilioni 1.1 kutoka katika Mpango wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Hayo yamethibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndugu Neema Maghembe.
''Nichukue nafasi hii kuishukuru Serikali yetu inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Joakim Mhagama na Mkurugenzi wa TASAF Taifa kwa kufanya jitihada za kuhakikisha fedha zinazopatikana kwa ajili ya Nchi yetu na sisi wananchi wa Songea Vijijini inatufikia nasi wataalamu kwa kushirikiana na Viongozi na wananchi tutahakikisha miradi tunaisimamia kwa weredi mkubwa ili ikamilike kwa ubora na viwango vinavyokubalika".
Aidha, fedha hizo zinatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo stendi ya kisasa ya Magari Parangu ambayo ipo katika hatua za umaliziaji inayotekelezwa kwa fedha kiasi cha shilingi Milioni 225.
Pia mradi wa Soko la Peramiho A ambalo limekamilika kwa asilimia 100 na tayari limeshaanza kutumika ambalo liligharimu fedha kiasi cha shilingi Milioni 185.
Vilevile nyumba za watumishi wa Zahanati ya Mdunduwalo ambayo inajengwa mbili kwa moja ipo katika hatua ya umaliziaji, vyoo matundu 6 na kisima kirefu cha maji inayogharimu fedha kiasi cha shilingi Milioni 170.9 na nyumba ya mganga mfawidhi wa hospitali ya Halmashauri iliyopo katika Kata ya Mpitimbi ambayo imekamilika kwa asilimia 100 na tayari imeshaanza kutumika imegharimu fedha kiasi cha shilingi milioni 68.
Pia Halmashauri ilipokea fedha kiasi cha shilingi 995,000 kwa ajili ya uboreshaji wa visima vya asili ambavyo vimesaidia wananchi kupata maji safi na salama na kwa asilimia kubwa vimeondoa changamoto ya upatikanaji wa maji Vijijini.
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea wameipongeza na kuishukuru Serikali kupitia TASAF kwa kuleta fedha hizo kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Maendeleo ambayo imeenda kutatua changamoto mbalimbali kwa wananchi.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa