Wakala wa barabara za Mjini na Vijijini kutumia Shilingi milioni 701 kujenga daraja kwenye mto Muhukuru katika Kata ya Muhukuru barabarani Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.
Meneja wa TARURA wa Wilaya ya Songea Mhandisi John Ambrose amesema ujenzi wa daraja ulitakiwa uanze Januari 4,2021 kutokana na changamoto za mvua mradi ulianza kutekelezwa mwezi Julai na unatarajia kukamilika mapema Januari 2022
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Muhukuru barabarani Mhe. Manfred Mzuyu amesema ujenzi wa daraja hilo utatoa fursa kwa wananchi kufungua mtandao wa mawasiliano na biashara kutoka sehemu moja kwenda nyingine hata nchi jirani ya Msumbiji.
Mhe.Mzuyu amesema ujenzi wa daraja hilo pia utarahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu ya upasuaji wa dharula kwa magonjwa ya kidoletumbo,mabusha,mshipangili na wenye uzazi pingamizi kwenye kituo cha afya cha Muhukuru Lilahi ambapo awali wananchi walikua wakipata tabu kufika kwenye kituo hicho.
Mzuyu ameongeza kwa kusema ujenzi wa daraja hilo utaimarisha usalama wa wanafunzi kuvuka kwa usalama hasa nyakati za masika kipindi ambacho mito mingi hujaa maji na kusababisha athari kwa wananchi na mali zao.
Mzuyu amesema mradi wa ujenzi huo ni kiunganishi cha Vijiji vitatu na Vitongoji vyake ambavyo ni Muhukuru barabarani,Mbiro na Mipeta kuelekea Kata ya Kizuka na Vijiji vingine.
Awali akikagua utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Mhagama amemshukuru Rais wa awamu ya sita Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha ya kujenga daraja ambalo litaimarisha uchumi wa wananchi.
Mhe.Jenista amewataka wadau wa ujenzi wa mradi huo kukamilisha ujenzi kabla ya Januari 15, 2022 ili wananchi waanze kunufaika na huduma hiyo
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery
Songea DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa