TAKWIMU ni dira katika upangaji wa shughuli za maendeleo ya uchumi .
Wananchi waliochaguliwa katika dodoso la sensa ya kilimo ,mifugo na uvuvi wametaki wa kutoa takwimu sahihi ili kuiwezesha serikali kupanga mipango sahihi ya kuendeleza sekta hiyo
Wito huo umetolewa na Bw Sellius Ngai Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma katika zoezi linalofanyika la dodoso la sensa ya kilimo ,mifugo na uvuvi katika Kijiji cha Mbinga Mhalule kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.
Ngai amesema Serikali kupitia ofisi ya Takwimu ya Mkoa wa Ruvuma inaendesha zoezi la dodoso la sensa ya kilimo,mifugo na uvuvi kwawananchi, hivyo watoe ushirikiano wa dhati katika kufanikisha zoezi hilo kwa kutoa majibu sahihi yatakayo wezesha serikali kupanga mipango ya kuendeleza sekta hiyo kiuchumi.
“Jambo lolote linalotekelezwa na serikali nyuma yake kuna takwimu” ,alisema Ngai
Amseema takwimu ni nyenzo inayotoa dira ya kupanga mipango ya maendeleo katika nchi yoyote dunia ,hakuna jambo ambalo linaweza kufanyika bila kuwepo na takwimu nyuma yake kama vile ujenzi wa miradi mbalimbali ,utoaji wa taarifa mbalimbali serikali hata upangaji wa makazi bora ya watu.
Kwaupande wake Meneja wa Takwimu wa Mkoa Ruvuma Mwantumu Uhenga amesema lengo la dodoso hilo ni kubaini idadi ya mifugo na changamoto zake,kilimo na changamomoto zake , wadudu wasumbufu na matatizo ambayo yanawakabili wakulima,upatikanaji wa masoko halikadharika kwenye uvuvi lengo likiwa serikali kuja na mipango madhubuti katika kuendelea sekta hiyo.
Amesema dodoso la sensa hiyo limeanza tangu Augosti tano mwaka huu na linategemea kukamilika Oktoba tatu mwaka huu ,na wanatarajia kuwafikia wakulima,wafugaji na wavuvi jumla ya kaya 1498 kwa Mkoa mzima na wameandaa madodoso matatu ambyo ni ya wakulima wakubwa,wakulima wadogo na dodoso la jamii na sensa hiyo inaendelea nchi nzima.
Wananchi walioteuliwa wamehaidi kutoa ushirikiano kwa maofisa wa Takwimu ambao wanaendesha zoezi hilo kwa dodoso lolote watakalotakiwa kutolea ufafanuzi wa kina.
Imeandikwa na
JACQUELEN CLAVERY
AFISA HABARI SONGEA ,DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa