Kamanda wa Taasisi ya kuzuia na kupambana rushwa Mkoa wa Ruvuma Hamza Mwenda amewarai wananchi kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa miradi ya mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO -19.
Mwenda ametoa rai hiyo katika kikao kazi cha kutoa taarifa kwa umma za utendaji kazi cha robo ya kwanza kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi hizo leo.
Mwenda amewarai wananchi kutoa ushrikiano wa kina katika kufanikisha zoezi hilo ikiwemo kuchukua hatua mahususi pale wanapoona kunadalili za ukiukwaji wa miongozo, sheria na viashiria vya rushwa katika utekelezaji wa miradi.
“Mkoa wetu ni miongoni mwa Mikoa iliyopokea mabilioni ya fedha za UVIKO-19 nitoe rai kwa wahusika waliopewa dhamana ya kusimamia miradi hiyo kuzingatia miongozo iliyotolewa na Serikali,” amesisitiza Mwenda.
Mwenda amewataka wahusika wote waliopewa dhamana ya kusimamia utekelezaji wa miradi kuhakikisha wanafuata miongozo sahihi ya matumizi ya fedha hizo, na kwa yoyote atakaye kiuka miongozo hiyo atachukuliwa hatua za kisheria.
Mwenda amesema katika kuzuia na kupambana na rushwa katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba mwaka huu TAKUKURU imepanga kutekeleza shughuli mbalimbali zikiwemo kuendelea kufanya ufuatiliaji katika makusanyo ya fedha za mapato ndani za Halmashauri kupitia utaratibu wa POS, kuelimisha umma na kufanya uchambuzi wa mifumo hasa katika maeneo yanayolalamikiwa na wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Neema Maghembe amesema Halmashauri imepewa mgao wa shilingi zaidi ya bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa kwa Shule za Msingi na Sekondari.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery
Songea DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa