Diwan wa kata ya litapwasi Mhe. Rajabu Mtiula, jana alimuomba Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe Jenista Mhagama kusaidia umeme kupatikana maeneo yote ya Kijiji cha Lyangweni.
“Mhe Mbunge kwanza tukushukuru sisi watu wa Litapwasi kwa namana unavyotujali , umetusaidia kupata maji kijijini kwenu, umetuchongea barabara na leo tunashukuru umeme umeweza kuingia kwenye vijiji vyetu ila tunaombi moja, baadhi ya maeneo bado umme haujafika, tunaomba utusaidie. Alisema Rajab Mtiula Diwani wa Kata ya Litapwasi
Wananchi wa Lyangweni wanahitaj umeme na wameniagiza nikuambie wewe wakiamuni wewe utasaidi kufika umeme kwa maeneo ambayo bado haujafika kama ulivyoleta maji na kutengeneza miundombinu.
Mwaka 2020 tuliahidi kuleta Umeme na maji hapa kijijin, umeme upo haupo? Maji yapo hayapo? Basi ndugu zangu tumshkuru sana Rais kwan mlivyoniagiza nami nimempelekea ametusaidia, na hilo ombi uliloniomba la kuhusu Umeme nalifanyia kazi na wote mtapa umeme, ambao bado hamjapata. Maeneo ambayo nguzo hazijafika nipo na Meneja wa Tanesco hata namuagiza kwanzia sasa afatilie ili Lyangweni yote umeme ufike.
Aidha Mhe Jenista alishukuru sana kazi inayofanywa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwawezesha wananchi wa Jimbo la Peramiho kupata miundombinu iliyobora lakini pia kuwapatia Mbolea ya Ruzuku wakulima wa Halmashashauri ya Wilaya ya Songea
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa