Madiwani na Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songea, wameweka mkakati rasmi kuingia kwenye kilimo cha umwagiliaji cha Mpunga. Hili limejidhihilishwa baada ya kuamua kwenda Mkoani Mbeya, kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ili kuweza kujifunza namana ya kuendesha kilimo cha cha Umwagiliaji cha Mpunga.
Waheshimiwa Madiwani na Wataalam wanatarajia kuelekea Mbarali, Mbeya kwa ziara ya kujifunza kwa vitendo namna ya kulima zao la Mpunga. Ziara hiyo inatarajiwa kuanza tarehe 22/02/2024 Ambapo itahusiwa Madiwani wote na baadhi ya Wataalamu kutoka Idara mbalimbali ikiwemo Kilimo, Mipango, Ardhi Wahandisi, Maendeleo ya Jamii nk.
Akizungumzia ziara hiyo Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Songea Mhe. Simon Kapinga alisema “ Lengo kubwa la Ziara hii ni kutaka kujifunza kwa vitendo Kilimo cha Mpunga cha Umwagiliaji. Sisi kama halmashauri kwa sasa asilimia kubwa la pato letu tunategemea zao la Mahindi, hivyo tukaona ni vema tuongeze wigo kwa kuliangalia na kuwekeza nguvu kwenye zao la Mpunga.
Tumeamua kwenda Mkoa wa Mbeya, Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kwa kuwa wenzetu wamejikita hasa kwenye zao la Mpunga. Wamebobea na wamewekeza nguvu na akili kwenye zao hilo Kaimu Mwenyekiti.
Wilaya ya Mbarali iko kwenye Bonde la Ufa la Mashariki ambalo hujulikana kama Bonde la Usangu lenye uoto wa asili aina ya Savanna. Kiikolojia bonde hili limegawanyika katika kanda tatu ambazo kila moja hupata mvua kwa kiwango tofauti kulingana na mahali ilipo juu ya usawa wa bahari.
Wilaya hiyo ina eneo lenye ukubwa wa Kilometa za mraba 16,000. Na katika eneo hili, asilimia 20 ya eneo hilo ambalo ni sawa na kilometa za mraba 3,215 ni kwa ajili ya Kilimo
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa