HALMASHAURI ya Wilaya ya Songea imefanya ziara ya mafuzo ya uchimbaji wa madini mkoani Geita tarehe 19 Septemba 2022.
Ziara hiyo imeudhuriwa na Viongozi wa Chama wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mheshimiwa Menasi Komba na Timu ya Wataalamu wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Neema Maghembe.
Lengo la ziara hiyo ni kujifunza utaalamu wa namna gani ya kutekeleza mradi wa uchimbaji wa makaa ya mawe unaotarajiwa kuanza hivi karibuni na taratibu za kufuata hili mradi uweze kwenda vizuri.
Akizungumza Mwenyekiti wa Mji Geita Mheshimiwa Constantine Morandi amewapokea na amewakaribisha viongozi wa chama pamoja na timu ya wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
‘’Sisi tulifarijika tulipopata taarifa kwamba mnakuja kutusalimia kwasababu usipopata wageni inakuwa huzuni lakini ukipata wageni ni faraja kwelikweli’’, amesema Mheshimiwa Constantine Morandi.
Kwaupande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Geita Ndugu Zahara Michuzi amewashauri pamoja na uchimbaji wa makaa ya mawe waanzishe na miradi mingine ambayo itaweza kuwaingizia mapato.
‘’Uzuri tulivyojigawa sisi hatuna Afisa Utumishi wala Afisa Mapato, swala la mapato ni kila mtu anawajibika, kila mtu ana chanzo na kila mtu anashauku ya chanzo chake kilete mapato makubwa kwa wiki mkifanya hivyo mtafika mbali sana’’, amesisitiza Ndugu Zahara.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni,
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Septemba 20, 2022.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa