Watumishi wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea ambao pia ni wadau wa michezo wamepokea mipira 6 ya michezo kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kuboresha kuimarisha michezo na miili yao kwa kufanya mazoezi
Akithibitisha kupokea mipira hiyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea Ndug.Makisio Chengula amekabidhi mipira hiyo na kuishukuru Serikali kuu kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma na kusema kwamba wamepokea mipira sita ambayo;- mipira 2 ya kikapu, 2 ya Pete na 2 ya miguu.. Ambapo amesema
" Nashukuru kwa muitikio wenu kama nilivyo waita, nimeona nichukue jukumu hili kubwa nitoe taarifa kwenu kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Songea imepokea mipira 6 lengo kubwa ni , kuboresha na kuinua michezo katika Halmashauri yetu,hivyo nimewaita ninyi kwaajili ya kuwakabidhi mipira hiyo pia kutoa hamasa ya michezo. Kwahiyo kama Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mkoa umetukabidhi mipira ya michezo ikiwa miwili ni ya miguu, miwili ya netball na miwili ya basketball"
Ndipo alipotoa wito kwa watumishi wa Halmashauri ya Songea kwa kuwataka mipira hiyo wakaitumie kama chachu ya ushirikiano mwema kati ya Halmashauri na vijiji vyote vinavyopatikana katika Halmashauri hiyo.
"Mipira hii Kwa kuwa tunawakabidhi ninyi Leo tunaomba mambo yafuatayo yakazingatiwe La kwanza Kwa kuwa Halmashauri yetu Bado ipo chini katika masuala ya michezo tunaomba wadau wote tuweze kushirikiana, tukiwa tunamaanisha sisi kama Halmashauri tunazo Kata mbalimbali pamoja na vijiji 56 tunaomba basi hii Iwe chachu kwenye Halmashauri yetu lakini nyinyi kama wadau wa michezo Bado mnanafasi ya kuitawanya na kuisambaza katika Halmashauri yote ya Wilaya ya Songea kwa kufanya michezo katika maeneo hayo.Jambo jingine najua ninyi ni watumishi na mnaratiba nyingi za shughuli mbalimbali za maendeleo hivyo pangilieni ratiba zenu vizuri ambayo itawawezesha kufanya kazi zenu na kupata nafasi ya kushiriki kufanya mazoezi" Alisema Makisio Chengula Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea
Nae Meneja wa timu ya Songea DC fc Hussein Hamidu akipokea mipira hiyo ameweza kuwashukuru wote waliohusika na msaada huo ikiwemo Serikali kuu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea kwa kuwakabidhi mipira hiyo ambapo amesema
"Binafsi kwaniaba ya timu ya Songea DC fc tunamshukuru sana Kaimu Mkurugenzi kwa kutukabidhi mipira hii ambayo itatuwezesha kuendeleza michezo katika ngazi ya Halmashauri na kushiriki mashindano mbalimbali kuanzia ngazi ya Halmashauri, Wilaya Hadi Taifa, kipekee tunakupongeza wewe pamoja na viongozi wengine wa Serikali kwa kuendeleza michezo mbalimbali, na hamasa kwa watumishi wa ngazi zote, kwa namna ya kipekee napenda kumshukuru Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Joakim Mhagama kwa kutupatia jezi ambazo zitatusaidia kuimarisha michezo, pia napenda kumshukuru Mwenyekiti wa Halmashuri kwa jitihada zake na kuipambania Halmashauri Aidha katika masuala ya michezo, pia Mhe.Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada zake kwa kutoa hamasa kwa watumishi kupenda michezo.
"Mwisho tunapenda kuwaahidi kufanya vyema katika mashindano mbalimbali ikiwemo Samia Cup pamoja na mashindano ya Serikali za mitaa ambayo yanatarijiwa kuanzaTarehe 18 octoba na ili kuwezesha hayo sisi kama watumishi wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea tumejiandaa kwa kujiimariaha kimazoezi, hivyo tunaomba wadau mbalimbali wa michezo kutupa ushirikiano kwa asilimia miamoja Alisema Hussein Hamidu Meneja wa Songea dc fc
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa