Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe. Kapenjama Ndile na Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songea wamekutana na wananchi wa Kijiji cha Liangweni ambacho ni miongoni kwa vijiji vitatu viliopo Kata ya Litapwasi Halmashauri ya Songea ili kutatua kero mbalimbali ikiwemo kero ya Mifugo ( Ng'ombe) waliomo Kijijini humo bila kufuata utaratibu na kwa kuwa wanaathili mazao ya wananchi.
Baada ya kusikiliza madukuduku ya wananchi, ambapo walipewa fulsa ya kueleze kero wanazopitia, asilimia kubwa ya wananchi walilalamika kuhusu uwepo wa Mifugo ambayo imekua ikiharibu mazao Yao.
Mhe. Mkuu wa Wilaya ametoa agizo Kwa Mwenyekiti wa Kijiji pamoja na Mtendaji Kutambua idadi ya Mifugo iliyoingia Kijijini humo bila kufuata utaratibu, na kuwabainisha wanakijiji wanaoshirikiana na wavamizi hao wanaoleta kero Kwa wananchi Kisha wawape notisi wote waondoe Mifugo yao kabla ya kufikia ijumaa tarehe 24/11/2023
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa