Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma imetua kiasi cha shilingi milioni 400 kujenga hostel tano kwa ajili ya wanafunzi wa kike kwa gharama ya shilingi 80 kwa kila jengo.
Afisa mipango wa halimashauri hiyo Athumani Nyange amesema fedha zilizotumka kutekeleza mradi huo zimetolewa na serikali kwa ajili ya kujenga hosteli katika shule ya Matimira, Kilagano,Maposeni,Mpitimbi na Mhalule
Nyange amesema Halmashauri ilipokea fedha Agosti 2020 kwa ajili ya ujenzi wa hosteli na kazi imekamilika kwa asilimia 90 kwa ajili ya kuanza kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa kinacho subiliwa ni matengenezo ya vitanda.
Elizabeth Mwakyusa ni mwanafunzi wa kidato cha sita sekondari ya Mpitimbi anatoa shukrani kwa serikali kwa kuwajengea hosteli kitendo ambacho kitawaongezea ari ya kusoma na kuongeza ufauru sambamba na kupunguza utoro ambao ulikuwa ukusababishwa na kutembea kwa umbali kutoka kwenye makazi yao.
Sailis Luoga ni mkazi wa Kijiji cha Mpitimbi pia ni mjumbe wa Bodi ya shule hiyo ameipongeza Serikali kwa ujenzi wa hosteli ambazo ni msaada mkubwa kwa wanafunzi wa kike, ameiomba Serikali kuendelea kuwasaidia kuwajengea miundombinu bora ya kutolea elimu
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Mpitimbi Patrick Matembo amesema mradi wa ujenzi wa hosteli hizo utasaidia kuendeleza ndoto za wanafunzi wakike ambao wamekuwa wakikabiliwa na vikwazo vya kutimiza ndoto zao ukilinganisha na wavulana.
Halmashauri ya wilaya ya songea inajumla ya shule za sekondari za 21 kati ya hizo tano zikiwa zinamilikiwa watu binfsi na Taasisi ya dini.
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa Habari
Songeadc
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa