Serikali imetoa Shilingi Bilion moja ( 1,000,000,000/=) Kujenga Chuo cha Walemavu Liganga katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea ikiwa ni majengo matatu yaanda Madarasa 10 yenye vyoo Vyoo 22, Bweni la Wanafunzi 80 lenye vyoo 18 na Nyumba ya watumishi Moja kwa tatu
Mh. Mbunge wa Jimbo la Peramiho alitembelea na kukagua ujenzi wa Chuo cha Walemavu kilichopo kata ya Liganga katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea, ambapo alikagua ujenzi wa Mabweni, Darasa pamoja na Nyumba ya Watumishi ambayo ni Moja kwa tatu
Chuo kilianza kujengwa 19/05/2024 na kilitarajiwa kuisha ( kukamilka ) mwishoni mwa mwaka 2023, yaani tarehe 31/12/2023, lakini bado hakijakamilika na mkataba umehuishwa ambapo kinatarajia kukamilika mwaka huu. Frola Mbilinyi Mtendaji wa kata ya Liganga
Aidha Mhe. Mbunge alipongeza uongozi wa Halmashauri pamoja na Diwani kwa kusimamia vema ujenzi wa chuo hicho na kuwaambia kuwa chuo hicho kitawaletea maendeleo makubwa kata ya Liganga na Halmashauri kwa ujumla
“ Niwaambie wananchi wa Liganga, kwanza tumshukuru sana Rais kwa kutujengea hiki chuo katika Halmashauri yetu. Chuo hiki kitawasaidia sana wananchi wa Liganya na Wilaya nzima ya Songea mana Watu wengi watakuja kutoka mikoa tofauti kusoma hapa.
Niwapongeze pia viongozi wote wa Halmashauri kwa namna mlivyosimamia ujenzi wa chuoa hiki, Nikupongeze pia Mhe. Diwani umepambana sana kwa ajili ya wananchi wa kata ya Liganga.
Hata hivyo Wananchi pia walimshukuru Mbunge kwa kutembelea na kukagua chuo hicho wakiamini ujio wake utakipa nguvu na mwendo chuo hicho kukamilika kwa wakati uliopangwa.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa