Ruzuku ilivyosaidia kubadili maisha ya kaya masikini.
Mpango wa kunusuru kaya masikini umesaidia kubadili maisha ya kaya zinazonufaika na mpango huo katika Halmashauri ya wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma kwa kuboresha upatikaji wa mahitaji mumhimu katika familia zao
Wameyasema hayo kwa nyakati tofauti walipo tembelewa na waratibu kutoka halmashauri ya wilaya ya songea hivi karibuni.
Kaya hizo zimesema taangu kuanzishwa kwa mpango huo mwaka 2015 mwezi juni wamenufaika kwa kuboresha upatikanaji wa mahitaji muhimu katika familia zao.
Petro komba na Nunu Ponera ni miongo mwa kaya zinazo nufaika na mpango huo wanasema tangu waingizwe kwenye mpango huo wameweza kubadili maisha yao kwa kukabiliana na baadhi changamoto zilizokuwa zikiwakabili kama vile matibabu,kusomesha watoto,kuanzisha miradi midogo modogo kama vile ufugaji,kuanzisha bustani ambazo wanalima mboga mboga.
Changamoto nyingine ambazo wameweza kutatua ni kujenga nyumba tofauti na zile za awali ambazo zilikuwa duni na zenye kuhatarisha maisha yao,kuchangia kiasi cha shilingi elfu kumi kwa mwaka kwa ajili ya bima ya matibabu.
Pamoja na kukabiliana na changamoto hizo wameomba serikali kuwaongezea ruzuku ili waweze kuboresha zaidi maisha na kuanzisha miradi ambayo itawasaidia kujikimu hatakama TASAF itasitisha utoaji wa ruzuku katika kaya hizo.
TASAF (Tanzania Social Action Fund) ni mfuko ulioanziswa mwaka 2014 ukiwa na lengo la kunusuru kaya masikini kwa kuwajengea uwezo wa kujinusuru na umasikini katika jamii kwakuwapa ruzuku na kuwaanzishia miradi midogo midogo ambayo wao wanaibua.
JACQUELEN CLAVERY-TEHAMA-HABARI
15/01/2019
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa