RUKSA kuendelea na biashara ya nyama ya nguruwe na mazao yake
Halmashauri ya wilaya ya songea mkoani Ruvuma imeondoa zuio lililowekwa kwa shughuli za uuzaji na ununuzi wa nguruwe na mazao yake kufuatia kuisha kwa ugonjwa wa homa ya nguruwe (AFRICAN SWINE FIVER).
Kuondolewa kw zuio hilo kumetolewa na Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Dkt ERICK KAHISE leo ofisini kwake
Dkt Kahise amesema maeneo yote ya Halmashauri yapo salama kutokana na kutokuwepo kwa homa ya nguruwe ,hivyo wananchi wanaweza kuendelea na biashara ya nyama ya nguruwe kama ilivyo kuwa awali.
Dkt kahise amesema pamoja na kuondoa zuio la kufanyabiasha hiyo ili kuendeleza usalama wa afya ya mifugo na kuzuia maambukizi mapya wafanyabiashara wanatakiwa kuzingatia, upimaji wa sampuli kutoka kituo cha uchunguzi wa magonjwa ya nguruwe wanao toka na kuingia,na cheti kuambatanishwa na kibali cha kusafirishia mifugo.
Ugonjwa wa homa ya nguruwe umeingia kanda za nyanda ya juu kusini mwaka 2010 ikiwemo mkoa wa Ruvuma.
imeandikwa na
JACQUELEN CLAVERY
AFISA HABARI
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa