Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri yaWilaya ya Songea kuhakikisha ujenzi wa vyumba kumi vya madarasa vinakamilika Novemba 30 kama ilivyopangwa.
KanaliThomas ametoa agizo hilo baada ya kukagua mradi wa vyumba vitatu vya madarasakatika shule ya sekondari Magagura ambavyo vimegharimu kiasi cha shilingiMilioni 60
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa ameupongeza uongozi wa Halmashauri hiyo kwa kusimamia vizuri miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo.
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan Katika Halmashauri yaWilaya ya Songea imetoa shilingi Milioni 200 kujenga madarasa 10 katika shule za sekondari.
Kukamilika kwa madarasa hayo kutapunguza uhaba wa madarasa katika shule za sekondari.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa