RC Mndeme amuagiza DC Mgema kuhakikisha TAKUKURU wanachunguza ujenzi wa zahanati 4
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Chiristina Mndeme amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Songea Pololeti Mgema ahakikishe TAKUKURU inafanya uchunguzi wa ujenzi wa zahanati 4 zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Mndeme ametoa agizo hilo katika mkutano maalumu wa baraza la madiwani la kujadili hoja na mapendekezo ya mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali za mwaka wa fedha 2017 /2018 kilicho fanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea hivi karibuni.
Mndeme ametoa agizo hilo kutokana na kutoridhishwa na matumizi ya shilingi milioni 400 zilizotolewa na serikali kwa ajiri ya kukamilisha ujenzi wa zahanati hizo na kuisababishia serikali hasara, zahanati hizo ni Mpingi,Lipaya,Lugagara na Nakahegwa.
Ametaka uchunguzi ufanyike na kupewa majibu, watakao bainika kukiuka sheria ya manunuzi na sheria ya fedha za mamlaka ya serikali za mitaa atawachukia hatau kisheria.
Ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kupata hati safi ya mahesabu ya fedha Serikali kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2017 /2018 uliomalizika juni 30,sambamba na pongezi hizo amewataka madiwani kusimamia na kuhakikisha hoja 63 za tangu mwaka 2012 hadi 2018 ambazo hazijajibiwa,zinajibiwa.
“wataalamu utendaji wenu wa kazi ulenge kuzuia hoja na sio kujiandaa kujibu hoja”,alisema Mndeme.Kuzuia hoja kutasaidia mlundikano wa hoja ambazo hazifanyiwi kazi,kufanyiwa kazi.
Aidha afisa masuhuri achukue hatua kwa mtumishi yeyote atakae toa taarifa za uongo kuhusu ukusanyaji wa mapato au kushiriki kuhujumu ukusanyaji wa mapato ndani ya Halmashauri,Halmashauri ya Wilaya ya Songea imepiga hatua kubwa katika ukusanyaji mapato hadi juni 30 / 2018 kwa kufikia asilimia 72.
MWISHO.
JACQUELEN CLAVERY -KAIMU AFISA HABARI SONGEA DC
10 /07 /2019.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa