Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amezindua minada wa ununuzi na uuzaji wa mazao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kwa msimu wa mwaka 2019 /2020.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Chistina Mndeme amezindua minada ununuzi na uuzaji wa mazao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kwa msimu wa mwaka 2019 /2020 huku akiviagiza Vyama vikuu vya Ushirika TAMCU na SONAMCU na vyama vya msingi (AMCOS) kutatua changamoto ya vifungashio kwa lengo la kuwaondolea adha wakulima.
Rc Mndeme amefanya uzinduzi huo April 24 ofisini kwake
Amesema kwa msimu uliopita Mkoa umepata mafananikio makubwa kwa wakulima kuongeza kipato ambapo ufuta zaidi ya kilo milioni 8 ziliuzwa na wakulima kupata zaidi ya sh.bilioni 24, kwa wastani wa bei ya sh. 2,959, soya zaidi ya kilo milioni 2 ziluzwa na wakulima kupata zaidi ya sh.bilioni 2, kwa wastani wa bei ya sh.750, huku mbaazi kilo 773,543 kwa wastani wa bei ya sh.700 kwa kilo na kupata zaidi y ash.milioni 543.
Mndeme amesema kwa msimu huu Mkoa unatarajia kuuza na kununua ufuta tani 12,108,soya na mbaazi tani 17,711 ambapo hakuta kuwa na bei elekezi kwa mazao hayo isipokuwa serikali kwa kushirikana na wadau watahakikisha bei inakuwa ya kumnufaisha mkulima .
“Mkoa umejipanga kutekeleza utaratibu wa mnada kwa kufuata maelekeazao ya serikali kwalengo la kuleta tija katika mnada na mkulima ananufaika”, alisema Mndeme
Ametaja ratiba ya minada kuwa siku ya Jumatatu mnada utafanyika Songea,siku ya Jumatano mnada utafanyika katika Wilaya ya Namtumbo na Tunduru utafanyika siku ya Alhamisi huku akiweka msistizo ya kwamba mnada uhusishe watu wachache kwakuzingatia janga la virus vya Corona.
JACQUELEN CLAVERY
K/ AFISA HABARI SONGEA DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa