Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bregedia Jenerali Balozi Wilbert Ibuge amezindua mikakati ya kuinua kiwango cha taaluma katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma lengo likiwa ni kuinua kiwango cha taaluma na ufaulu.
Akizundua mikakati hiyo Balozi Ibuge ametoa wito kwa viongozi wa elimu kutenga siku moja katika mwaka kwa nia ya kujadili mafanikio na changamoto katika sekta ya elimu na kuzitafutia ufumbuzi kwa pamoja na kiwango cha elimu kiweze kuongeza.
Wakati huo huo Balozi Ibuge amewakumbusha wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kujiandaa kuhesabiwa ifikapo mwezi Agosti katika zoezi la Sensa ya watu na makazi sanjari na kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya UKIMWI na UVIKO-19
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Neema Maghembe amesema uzinduzi wa mikakati hiyo umekuja baada ya Halmashauri hiyo kwa muda wa miaka mitatu mfululizo ufaulu wake kushuka.
Bi.Maghembe ameitaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kufanya ufuatiliaji wa stadi za kusoma,kuandika na kuhesabu kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na lapilli,kuhamasisha wazazi na jamii kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula cha mchana shuleni na kutoa zawadi na motisha kwa walimu na wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo.
Naye mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Menas Komba amehaidi kusimamia mikakati hiyo ya elimu na kuhakikisha inatoa matokeo cha chanya ili mradi tu kila mtu atomize wajibu wake kwakuzingatia taratibu, kanuni na sheria.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wa Wilaya ya Songea Nelly Duwe amempongeza mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Jenista Mhagama kwa jitihada za dhati za kufuatilia na kusimamia maendeleo ya jimbo lake.
Kauli mbiu “Elimu bora inawezekana timiza wajibu wako.”
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery
Songea dc
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa