Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Balozi Wilbert Ibuge ametembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa ya UVIKO-19 na kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wake katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
“Mkurugenzi nimeridhishwa na kazi inayoendelea kufanyika,”amesema Balozi Ibuge.
Balozi Ibuge ametembelea na kugagua miradi ya Mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa wa mapambano dhidi ya UVIKO-19 ambao ni ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule za Sekondari na Msingi ambayo yanajengwa Mkoa mzima.
Balozi Ibuge ametembelea Shule ya Sekondari Jenista Mhagama iliyopo Kata ya Parangu,Kijiji cha Parangu,Shule ya Sekondari Maposeni ambako panajengwa vyumba 10 vya madarasa,na Shule ya Sekondari Mpitimbi ambako vinajengwa vyumba viwili vya madarasa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi.Neema Maghemba amesema ujenzi wa majengo hayo asilimia kubwa yamefikia hatua ya upauaji na mengine yapo hatua ya ukamilishaji ili yaweze kukabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Songea kabla ya Desemba 10.
Maghembe amesema Serikali imetoa Shilingi Bilioni 1.3 ambapo kiasi cha Shilingi Milioni 920 zinatumika kujenga vyumba 46 vya madarasa kwa Shule za Sekondari na kiasi cha Shilingi Milioni 380 zinatumika kujenga vyumba 19 vya madarasa katika Shule shikizi tu ambazo ni Lunyele,Jenista,Mhimbasi,Lihuhu na Ligunga na kufanya jumla ya vyumba 65 vya madarasa kwa Halmashauri nzima.
Maghembe amemshukuru Rais wa awamu ya sita Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa ambavyo zitatatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.
Halmashauri ya Wilaya ya Songea inajumla ya Shule za Msingi 75 kati ya hizo za Serikali ni 73, Shule moja inamilikiwa na Taasisi ya dini na moja inamilikiwa na mtu binafsi, na Shule za Sekondari 21 kati ya hizo Shule tano zinamilikiwa na watu binafsi na Taasisi za dini.
Imeandaliwa na Kuandikwa na
Jacquelen Clavery
Songea DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa