Rais Magufuli kuanza ziara ya kikazi mkoani Ruvuma kesho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya sikuta tano mkoani Ruvuma kuanzia Aprili 4,2019 .
Akizungumza na wanahabari ofisini kwake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Godfrey Zambi amesema akiwa mkoani Ruvuma Dkt Magufuli atapokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa na chama cha Mapinduzi Ikulu ndogo Tunduru na kwamba atazindua na kuweka mawe ya msingi katika Miradi iliyopo kila wilaya yenye ya thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 519.
Ameitaja Miradi atakayo zindua ni barabara ya Namtumbo-kilimasera,Matemanga-Tunduru ,chuo cha VETA Namtumbo,mradi wa kusafirisha umeme kutoka Makambako –Songea Kituo cha Afya Madaba na kiwanda cha kuchakata sembe cha Kikosi cha 842 kj Mlale.
Miradi atakayowekewa jiwe la msingi ni ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya mbinga –Mbambabay,barabara za lami Manispaa ya songea na hatimaye ataweka jiwe la msingi katika kituo cha mabasi kinachojengwa shule ya Tanga Manispaa ya songea.
Dkt Magufuli atafanya mikutano ya hadhara tarehe 06/04/2019 katika uwanja wa majimaji Manispaa ya Songea ambapo tarehe 08/04/2019 ataongea na wananchi wa Wilaya ya Nyasa na tarehe 9/4/2019 ataongea na wananchi wa Madaba.
Rais Dkt Magufuli anatarajia kukamilisha ziara yake Mkoani Ruvuma tarehe 09/04/2019 na kuelekea mkoani Njombe.
JACQUELEN CLVERY –SONGEA DC. APRILI 03-2019
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa