Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amevitaka vikosi vya majeshi nchini kuiga mfano wa utendaji kazi wa jeshi la Kujenga Taifa na jeshi la wananchi waTanzania
Rais ameyasema hayo wakati anazindua kiwanda cha kuchakata mahindi cha kikosi cha 842 KJ cha Mlale JKT kilichogharaimu zaidi ya shilingi milioni 400,kilichopo katika kijij cha Masangu Kata ya Magagura Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
RAIS Magufuli amesema vikosi vya majeshi nchini viige mfano wa utendaji kazi wa Jeshi la Kujenga Taifa na Jeshi la Wananchi w Tanzania kwa kujenga viwanda ambavyo vinasaidia kuinua uchumi wa viwanda .
Rais Magufuli amesema ujenzi wa viwanda vikiwemo vya kuchakata mahindi na mazao mengine vitaidi kuinua uchumi wa nchi,pia uwepo wa viwanda hivyo utasaidia upatikanaji wa soko la uhakika la mahindi na upatikanaji wa chakula cha kutosha kwa wananchi.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Jenerali Venance Mabeyo amesema lengo la kuanzisha kiwanda hicho ni kupata kipato na kukuza uchumi kwa kujenga uchumi wa viwanda.
Amesema uanzishwaji wa kiwanda hicho ,utakuwa chachu ya maendeleo kwa watu binafsi kuanzisha viwanda na kutumia fursa za kiuchumi kudumisha amani.
Kiwanda cha kuchakata mahindi cha JKT Mlale kina uwezo wa kuchakata tani zaidi ya 300 za sembe na tani zaidi ya 100 za pumba ambazo zinaweza kutengenezwa chakula cha wanyama.aidha Jeshi la Kujenga Taifa linatarajia kujenga kiwanda cha kuchakata korosho,kiwanda cha kuchakata alizeti Manyara na kiwanda cha kuchakata kahawa Itende Mbeya.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa