Naibu Waziri, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknologia ya Habari Eng. Maryprisca Winfred Mahundi, leo 4/06/2024 ametembelea Halmashauri ya Songea Kata ya Maposeni na kuzindua Mradi wa Ujenzi wa Minara miwili ya Mawasiliano katika kijiji cha Maposeni na Mdunduaro.
Mhe. Mahundi amewatoa hofu wananchi wa jimbo la peramiho kwa kuwahakikishia kwamba, Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknologia ya Habari wamepokea maelekezo kwa ajili ya kutatua kero hiyo na sasa kazi inaanza rasmi kuhakikisha wananchi wote wanapata Mawasiliano ya Uhakika.’
“kama mmemsikiliza vizuri meneja wa Mkoa, tayari kazi kubwa imefanyika, Mkongo wa Taifa upo hapa Maposeni. Na hayo ndio maagizo ya Dkt Samia Suluhu Hassan, maagizo haya alimpatia Mhe, Nape Nauye, na sisi wasaidizi wa Nape tumesema hatutalala tutatembea usiku na mchana tunataka kuhakikisha Mnara huu wa Maposeni unasaidia wananchi wa Jimbo la Peramiho. Alisema Eng Mahundi Naibu Waziri, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknologia ya Habari
Minara hiyo inategemea Kuanza na kumalizika ndani ya siku hamsini kuanzia leo, lengo ikiwa ni kuhakikisha Mawasiliano yanapatikana katika Halmashauri yote ya Wilaya ya Songea akizungumza mbele ya Naibu Waziri, Meneja wa TTCL Mkoa wa Ruvuma amesema
“ Eneo hili la Maposeni, utajengwa Mnara ndani ya siku hamsini kuanzia leo utakua umekwisha kamilika kwa maana kwamba mkandarasi amekwisha patikana vifaa vyote vimeshapatikana kwahiyo tunachotegemea sisi kama shirika ni utekelezaji”
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe. Kapenjama Ndile, ameyataja maeneo mbalimbali katika halmashauri ya Wilaya ya songea ambayo yamekua na changamoto za mtandao na kumuomba Mhe. Naibu Waziri kwa ujio wake kusaidia utatuzi wa changamoto hizo za mawasiliano katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
“ vijiji kama Litowa, Maposeni Mdundualo na vijiji vingine vingi vinamawasiliano dhaifu. Kwahiyo Mhe Naibu Waziri ujio wako hapa kwa wananchi wa Songea hasa Songea vijijini pamoja na Madaba wanamatarajio makubwa sana kwamba maelekezo yako yataleta chachu na kasi mpya katika ujenzi wa Minara na miundombinu ya mawasiliano kwa Ujumla” alisema Mhe. Ndile
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa