Naibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Hamad Hassan Chande ameipongeza kampuni ya AVIV Tanzania iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma kwakuajiri watumishi wazawa.
Mhe.Chande ametoa pongezi hizo alipofanya ziara ya kuitembelea kampuni hiyo na kuzungumza na watumishi wa Kampuni hiyo hivi karibuni.
Kampuni ya AVIV Tanzani ni kampuni ya muwekezaji aliyewekeza kwenye kilimo cha zao la kahawa aina ya Arabika ambapo asilimia 99 ya watumishi wake ni Watanzania jambo ambalo linatoa fursa kwa wananchi kunufaika na mradi huo.
Ametoa wito kwa Kampuni hiyo kuendelea na harakati za kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti rafiki ya maji na kulinda vyanzo vya maji.
”Hali sio nzuri katika utunzaji wa mazinzingira watu wanavamia misitu wanachoma mkaa ,wanafuga holela holela,wanajenga kwenye vyanzo vya maji,wito wa Serikali ni kuhakikisha kwamba utunzaji wa mazingira unalindwa kwa gharama yoyote kwa kupanda miti na kutoa elimu kwa wananchi kusudi watunze vyanzo vya maji na mazingira “,alisisitiza Mhe,Chande
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Songea Pololet Mgema amesema uharibifu wa mazingira unaenda sambamba na ongezeko la binadamu,na ongezeko la binadamu ni matokeo ya ongezeko la shughuli za kibinadamu ambazo baadhi ya shughuli hizo zimekuwazikisababisha uharibifu wa mazingira.
”Kazi ziendelee na utunzaji wa mazingira uendelee “,amesema Mgema.
Amesema kufutia hali hiyo yeye kama kiongozi ameanza kuchukua hatua ya kutoa elimu kwa wananchi wake waweze kutambua umuhimu na athari za uharibifu wa mazingira zitakavyotuathiri pasipo kuchukua tahadhari.
Kampuni ya AVIVl Tanzania inamiliki shamba lenye ukubwa wa ekali 1012 ambazo zinalimwa kahawa aina ya Arabika na ni miongoni mwa mashamba makubwa katika uwekezaji wa zao la kahawa kwa Afrika Mashariki na kati.
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery
Kaimu Afisa Habari – Songea DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa