Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameupokea Mwenge wa Uhuru leo 08/06/2023 katika Wilaya ya Tunduru kijiji cha Sauti moja. Kanali Ahmed ameupokes mwenge huo ukitokea Mkoa wa Mtwara.
Mkuu wa Mkoa ameupokea Mwenge huo na sasa rasmi upo Mkoani Ruvuma na utakuwepo kwa siku nane (8) ukipitita Wilaya zote na kukagua miradi ya ya Maendeleo kwenye Halmashauri zote Nane zilizopo Mkoa wa Ruvuma.
Viongozi mbalimbali wa Mkoa, Wilaya na Halmashauri, wamefika Wilayani Tunduru kwa ajili ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.
Mapokezi hayo yamefanyika leo katika viwanja vya Shule ya Msingi Sauti Moja iliyopo Wilayani Tunduru, ukitokea Mkoa wa Mtwara huku wawakilishi kutoka kila Halmashauri zilizoko mkoa wa Ruvuma walikuwepo wakishuhudia.
Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoa wa Ruvuma, utatembea umbali wa kilometa 1289.50 kwa mchanganuo ufuatavyo;- Tunduru Km 284, Namtumbo Km 170, Songea Vijijijni 134.80 Mbinga DC Km 110, Nyasa Km 186, Mbinga Mji 140, Manispaa Km 28.20 na Madaba km 165.
Aidha Mwenge huo kwa ujumla utatembelea Miradi 72 kwa mkoa mzima yenye thamani ya zaidi ya bilion 46 na baada ya hapo tarehe 16/06/2024 Mwenge wa uhuru utakabidhiwa katika Mkoa wa Njombe
Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mwenge unatarijia kufika tarehe 10/06/2024 ambapo utapokelewa Kata ya Mpitimbi kijiji cha Lipaya na Utakesha kata ya Peramiho
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa