Afisa Shughuli wa Chama Kikuu cha Ushirika cha SONAMCU Zamakanaly Komba amehairisha mnada wa pili wa Kitaifa wa kuuza na kununua zao la ufuta kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kwa wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.
Mnada huo ulipangwa kufanyika leo katika soko la Nafaka la “OTC” lililopo eneo la Namanditi Manispaa ya Songea.
Komba amesema amehairisha zoezi hilo baada ya wakulima kutoridhishwa na bei ya shilingi 2,210 kwa kilo moja ukilinganisha na gharama halisi za uzalishaji na uandaji wake ambapo wakulima wanadai wastani wa bei uanze na shilingi 3000 hadi 2500 kwa kilomoja.
Wakizungumza kwa niaba ya viongozi wenzao Viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) wamedai “ sisi tupo tayari mnada upelekwe mbele ili wanunuzi wakatafakari bei wanazopendekeza na wakaongeza kiwango”, walisisitiza.
Komba ametangaza mnada wa mazao yanayouzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani utafanyika kila siku ya Jumatatu kwa Halmashauri ya Wilaya ya Songea na endapo wakulima hawatakubaliana na bei zoezi litaendelea kupelekwa mbele.
Mnada wa kwanza nchini umefanyika Mkoani Songwe kwa mfumo wa stakabadhi ghalani na Ruvuma ni ya pili kwakuzindua kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2020/ 2021.
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa