MKUU WA WILAYA ATEMBELEA HIFADHI YA MILIMA LIHANJE
Mkuu wa Wilaya ya Songea pamoja na wataalamu wa misitu (TFS) amefanya ziara katika hifadhi ya milima ya Lihanje ambayo pia ni chanzo cha maji iliyopo kijiji cha Lugagara Kata ya Kilagano Halmashauri ya Wilaya ya Songea na Kujionea hali ya uharibifu wa hifadhi hiyo iliyofanywa na wananchi.
Kufuatia ziara hiyo Mkuu wa Wilaya Songea ameahidi Kurudi katika kijiji hicho na Kufanya mkutano wa hadhara na wananchi ili kufikia mwafaka wa hifadhi hiyo.
Awali kabla ya kwenda katika hifadhi hiyo Mkuu wa Wilaya alifika katika Ofisi ya kijiji cha Lugagara na kutoa maagizo kwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho ambapo amesea
“ Leo tumefika katika kijiji hiki na kujionea hali ya hifadhi ya milima Lihanje lakini nimesiki kwamba kuna wananchi wanafanya uharibifu kule sasa wapeni taarifa kwamba wasiendelee kufanya shughuli hizo huko wahame na waachane na kilimo cha kwenye Milima mpaka serikali itakapokuja kufanya maamuzi ya kuwatengea eneo lingine la kilimo”
Pia mkuu wa Wilaya ya Songea ameahidi ndani ya wiki hii atatuma wataalamu wa misitu na wataalamu wa ardhi kwenda kutathmini eneo ambalo wananchi watapatiwa kama eneo mbadala wa eneo la hifadhi kwaajili ya kufanya shughuli zao za uzalishaji mali.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa