Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewaomba viongozi wa kimila kutumia mamlaka waliyonayo katika kulinda na kuenzi utamaduni na desturi za jamii zetu wakati akihutubia wananchi wa Kata na Kijiji cha Maposeni baada ya zoezi la usimikaji wa waandamizi wa Chifu wa Kingoni Emmanuel zulu Gama.
Tukio hilo limefanyika leo tarehe 22/11/2023 ambapo waandamizi wa Chifu wanne wamesimikwa leo ambao wanatoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Songea ambao ni Mputa Gama, Hawayi Gama, Mgendela Bin Thobias na Songea Mbano.
Ambapo mkuu wa Mkoa wa Ruvua amesema anatambua uwepo wa mila nadesturi na mchango wake katika jamii yetu, amesema
“Kabla ya ujio wa wakolini tunakumbuka tulikuwa tukiishi au tukiongozwa na machifu ambapo Chifu alikuwa anauongozi wake mpaka kwenye kaya kama ilivyo sasa mkubwa wetu ni Raisi lakini uongozi wa mwisho kabisa ni Balozi hivyohivyo wazee wazamani waliishi hivyo kwahiyo tukio lililotokea leo hii ni ngeni kwa kizazi cha sasa lakini kwa miaka ya nyuma ndivyo walivyokuwa wakiishi mababu zetu”
Lakini kama alivyotangulia kusema Chifu wa wangoni Emmanuel Gama kwamba nyinyi mmesimikwa leo kwaajili ya kushauri mambo ya maendeleo ya kimila na kiutamaduni katika maeneo yetu kwahiyo niwaombe mkaifanye kazi hiyo ili kulinda utamaduni wetu wa Kiafrika dhidi ya utamaduni wa Kimagharibi ambao unaharibu mila zetu, Pia serikali inatambua sana mchango wa viongozi wa jadi hivyo msisite kushauri serikali pale ambapo hapako sawa kulingana na mila na desturi zetu”.
Nae Emmanuel Zulu Gama Chifu wa kabila la kingoni amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa ujio wake katika zoezi hilo la usimikaji wa waandamizi wa Chifu mkuu na kusema kwamba mila na desturi zichangie maendeleo ya nchi kwa ujumla, pia amewaomba waandamizi wake ambao amewasimika leo wasitumie mamlaka waliyonayo vibaya badala yake washirikiane na Serikali katika kuhakikisha wanaleta maendeleo chanya katika jamii iwe ya kiserikali au ya mila na desturi.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa