Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Songea Mwl. Neema Maghembe, amewataka Wakuu wa Divisheni na Vitengo kutenga bajeti zitakazoenda kutatua kero za wananchi kwa kutazama vipaumbele vya Serikali lakini pia katika kila Idara kuangalia namna gani Idara inajihusisha na jamii kwa kuweka mikakati itakayopunguza malalamiko kwa wananchi.
“ Niwasihi wakuu wa Divishen na Vitengo, kwa sasa ndo tupo kwenye maandalizi ya bajeti ya 2024/2025, hivyo basi huu ndo wakati sahihi wa kutengeneza bajeti zenu mkizingatia mahitaji ya wananchi wetu. Mhe Rais anafanya kazi kubwa sana kuhakikisha wananchi wanapata maisha bora, hivyo tumuunge mkono ili kuhakikisha dhamira yake kwa wananchi tunaitekeleza”
Mwl. Neema ameyasema hayo katika Mkutano maalumu wa Baraza la Wafanyakazi ambalo lilikutana kwa ajili ya kujadili na kupitisha Rasimu ya mpango wa Bajeti ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/2025, ambao ulifanyika tarehe 06/02/2024 katika ukumbi wa Halmashauri iliopo kijiji cha Lundusi- Peramiho
Halmashauri ya Wilaya ya Songea, kwa mwaka wa fedha 2024/2025 inakasimia kukusanya na kutumia kiasi cha TZS 28,766,811,612.00 ikiwa TZS 16,127,854,000 ni Mishahara, TZS 1,120,508,000.00 ni fedha kwwa ajili ya matumizi mengine kutoka serikali kuu (OC), Tshs 8,943,963,200.00 ni fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ( Tshs 4,695,638,000.00 fedha za ndani ( Serikali kuu), Tshs 3,841,364,000.00 fedha za nje ( Wafadhili) na Tshs 406,961,200.00 fedha za utekelezaji wa maendeleo kutoka Mapato ya ndani ya halmashauri)
Halmashauri inakadiria kukusanya na kutumia kiasi cha TZS 2,574,486,412.00 kutoka makusanyo ya mapato ya ndani ikiwa TZS 2,034,806,00 ni mapato halisi, TZS 539,680,412.00 ni mapato lindwa ambapo kiasi cha TZS. 1,627,844,800.00 ni fedha kwa ajili ya matumizi ya kawaida sawa na asilimia 80 na kiasi cha TZS 406,961,200.00 ni fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo sawa na asilimia 20 ya mapato ya ndani ya Halmashauri.
Aidha katika fedha za matumizi mengine katika mwaka wa fedha 2024/2025, Halmashauri ya Wilaya ya Songea inakusudia kutumia kiasi cha Tshs 1,576,250,000.00 kulipa stahiki mbalimbali za waheshimiwa madiwani na watumishi.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa