Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bi. Elizabeth Mathias Gumbo, jana 13/05/2024 alitembelea na kukagua miradi inayotekelezwa na Halmashauri na kuwataka wasimamiz na mafundi kuongeza kasi ili kukimbizana na muda.
Bi Elizabth ameyasema hayo baada ya kukagua ujenzi unaoendelea kwa katika Miradi saba tofauti iliyopo Halmashauri, pamoja na mambo mengine Mkurugenzi amesisitiza umakini, na spidi kwa mafundi na wasimamizi wa miradi ili kuendana na kasi anayoihitaji
“ niwasisitize sana, kwa sasa tupo nyuma ya muda, tunayo pesa ya kutosha hivyo kwa wale wote wanaosimamia miradi hakikisheni mnashinda site na kuhakikisha mafundi muda wote wapo Site, vifaa vipo na kazi zinafanyika” Gumbo
Miradi aliyokagua ni pamoja na Shule ya Sekondari Maposeni ambapo alikagua Ujenzi wa Jengo la Utawala lililotengewa fedha kiasi cha shilingi milioni sabini na nne na laki sita 74,600,000/= kutoka mradi wa SEQUIP, Ujenzi wa Madarasa kumi na saba ( 17) yenye thamani ya Shilingi Milion mia nne na nane ( 408,000,000/=) kutoka Serikali kuu pamoja na Matundu 25 ya vyoo yenye thamani ya shilingi million Arobaini na nne ( 44,000,000/=)
Shule ya Sekondari Jenista Mhagama, alipita na kukagua ujenzi wa Madarasa kumi ( 10) utakaogharimu fedha kiasi cha Shilingi million mia mbili aroboini (240,000,000) na Matundu ya Vyoo kumi na Tisa( 19) yenye thaman ya Shilingi milioni thelathini na tatu ( 33,000,000) kutoka Serikali kuu
Aidha Mkurugenzi alitembelea na kukagua ukarabati wa Madarasa Saba (7) yenye thamani ya Shilingi Milion Mia moja Themanini, fedha kutoka Serikali kuu, na Ujenzi wa Bweni katika shule maalumu ya msingi mnyonga, ujenzi huo umetengewa kiasi sha shilingi Milioni miamoja na ishirini na nane ( 128,000,000)
Mkurugenzi ameendelea kuishukuru Serikali ya awamu ya Sita ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa fedha hizi ambazo amekua akizitoa kwa ajili ya wananchi na watanzania kwa kuwajengea Madarasa, Mabweni na Matundu ya Vyoo ambayo yatakidhi mahitaji ya wanafunzi
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa