HELLO PERAMIHO!
Mji wa Peramiho ni miongoni mwa miji ya kihistoria ilipo Tanzania, ina inamajengo ya Kihistori yanayoutambulisha Mkoa wa Ruvuma, hasa Wilaya ya Songea.
Ujenzi wa Majengo hayo ya Tofari za kuchoma imekua kivutia kingine kwa wakazi wa hapa, hasa uwepo wa kanisa ambalo ni moja kati ya makanisa makubwa Afrika, Mji huu ulijengwa na Mjeruman kipindi cha Ukoloni Mwaka 1890, lipo Tanzania, Mkoa wa Ruvuma Halmashauri ya Wilaya ya Songea kata ya Peramiho.
Historia ya mji wa Peramiho uliopo kilometa 24 tu kutoka makao makuu ya mkoa wa Ruvuma Songea inaunganishwa na wabenediktini wa kanisa katoliki kutoka St.Otilia nchini Ujerumani, ambao waliamua kuweka makao makuu yao katika Abasia ya Peramiho.
Uwepo wa majengo hayo umesaidia upatikanaji wa huduma mbalimbali zinatolewa ambazo zimekua zikisaidia wananchi wa Mkoa wa Ruvuma hasa kata ya Peramiho, Huduma kama Kanisa Hospitali ( St. Joseph peramiho Hospital), Shule ya sekondari ( Peramiho Girls) Ukumbi wa mikutano Hotel nk
Jengo hili lipo kilometa chache na lilipo Jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea ikumbukwe pia ndipo lipo katika jimbo la Mhe Jenista Mhagama, Mbunge wa Peramiho na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa