HALMASHAURI ya Wilaya ya Songea ni moja kati ya Halmashauri zilizopo kwenye mpango wa kutekeleza mpango wa kunusuru Kaya Maskini ambao unahusisha kipengele cha mradi wa Ajira za muda hivyo Walengwa huongezewa kipato kwa kufanya kazi za ujira wa muda kupitia miradi iliyoibuliwa katika Vijiji vyao.
Mratibu wa TASAF Bi. Hossana Ngunge kwa kushirikiana na Timu ya Wataalamu wamefanya ufuatiliaji wa miradi hiyo ya Ajira za muda inayotekelezwa katika Vijiji vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Moja kati ya miradi iliotembelewa ni mradi wa utengenezaji wa paving katika shule ya sekondari Maposeni na Jenista ambapo zitapangwa katika eneo la mstarini hivyo mradi huu unaenda kuondoa changamoto ya vumbi.
Vilevile wametembelea mradi wa ujenzi wa kivuko uliopo katika Kijiji cha Nguvumoja ambapo kivuko hicho kinawasaidia wananchi kuvuka toka sehemu moja hadi nyingine.
Pia wamefatilia mradi wa uboreshaji wa kisima cha asili kilichopo katika Kijiji cha Nguvumoja ambapo kupitia mradi huu Wananchi wanaenda kupata maji safi na salama.
Mwisho wamefanya ufuatiliaji katika Kijiji cha Serekano ambapo walengwa waliibua mradi wa upandaji wa miti ya matunda aina ya Parachichi.
Kufuatia utekelezaji wa miradi hiyo Wananchi wameipongeza na kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama kwa kuanzisha utaratibu wa miradi ya Ajira ya muda ambapo wamesema licha ya kuinua kipato chao lakini pia miradi hiyo imetatua shida mbalimbali.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa