Serikali ya Awamu ya Sita imedhamilia kujenga Barabara ya ubora yenye thamani ya TSH. 198,000,000 kutoka kata ya Matimila kijiji cha Kikunja hadi Ndongosi katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea nda I ya mwaka wa fedha 2024/2025
Waziri wa Nchi ofisi za Waziri Mkuu, ( Sera Bunge na Uratibu) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe Jenista Joakim Mhagama amesema Serikali imedhalia kuwajengea Barabara wananchi nwa kata ya Matimila ili kuwaondolea usumbufu wananoukutana nao wa usafiri.
Mhe Jenista ameyasema hayo baada ya Wananchi kuibua hoja hiyo kwenye mkutano na kuelezea namna wananvyopata changamoto ya usafiri kwa kuzunguka sana ili kufika Ndongosi, na sehem nyingine.
“ nimeskia kilio chenu, na tabu mnayoipata ya usafiri na barabara mbaya katika safari zenu, uzuri nipo na Mkandalasi wa barabara Mhandisi. Simoni Binam Hapa, hivyo namuagiza waanze michakato kwani Serikali itatoa fedha kwa ajili ya Barabara ya Kikunja hadi Ndongosi na inapaswa kuanza katika mwaka huu wa fedha ”
Aidha Mhe. Mbunge aliagiza pia watu wa TANESCO wahakikishe mpaka tarehe 29/07/2024 wawe wamewasha Umeme katika kijiji cha Kikunja.
“ Niwaambie kitu! Sasa kikunja itakua mjini maana nimemuagiza Meneja wa Tanesco mpaka mwishoni mwa mwezi wa Saba yaani tarehe 29/07/2024 umeme uwe umewaka katika kijiji xcha kikunja na vitongoji vyake”’Mhe Jenista
Ziara ya Mbunge imeendelea kuwa kivutio kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, baada ya kuendelea kutatua jkero za wananchi wa kata mbalimbali zilizopo Songea vijijini
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa