MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mheshimiwa Menasi Komba amezindua maadhimisho ya siku ya wazee duniani tarehe 27 Septemba 2022 ambayo kilele cha maadhimisho hayo ni tarehe 1 Octoba 2022.
Uzinduzi huo umefanyika katika Kata ya Peramiho Kijiji cha Peramiho A ukumbi wa Mkuwa Wilaya ya Songea.
Akizungumza katika uzinduzi huo amewataka Viongozi na wataalamu waunde mabaraza ya wazee kuanzia ngazi ya Kitongoji kwaajili ya kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wazee kwa haraka.
Aidha amesisitiza wazee waendelee kupewa kipaumbele katika vituo vya kutolea huduma za afya na dhana ya wazee kwanza iweze kuimarishwa Zaidi.
‘’Sisi kama Halmashauri tunawajali sana wazee hivyo tunawaahidi kutatatua changamoto zote zinazowakabili na tunampango wa kutengeneza Sheria za mtoto kumtunza mzazi hiyo yote ni kuhakikisha mnaishi katika mazingira mazuri’’, amesisitiza Mhe.Menasi.
Kwaupande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndugu Neema Maghembe ambae amewakilishwa na Afisa Maendeleo ya Jamii Zawadi Nyoni amewashauri wazee wanawake wajiunge katika vikundi vya wanawake ili waweze kupata mikopo na kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Nae Mwenyekiti wa baraza kuu la wazee Mkoa wa Ruvuma Elenzian Nyoni amewapongeza wazee kwa kushiriki kikamilifu Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
Pia ametoa rai kwa wazee kuendelea kujitokeza kwa Wingi katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kupata chanjo ya Korona.
Wakizungumza wazee wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea wameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwatatulia changamoto zinazokabiliwi ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama.
Pia wamewashukuru Viongozi wa Chama wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mheshimiwa Menace Komba, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Neema Mghembe na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe.Pololet Mgema.
Katika maadhimisho hayo yalisindikizwa na maonesho ya Kilimo cha uyoga pamoja na upimaji wa magonjwa ya sukari na presha kwa wazee.
Kauli mbiu ni Ustahimilivu na mchango wa Wazee ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni,
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Septemba 28, 2022.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa