WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama amezindua mradi wa umeme Vijijini.
Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 11 Julai 2023 katika kijiji cha Litowa Kata ya Parangu.
Mheshimiwa Mbunge ametoa wito kwa Wananchi kutumia vizuri mifuko ya kuwezesha upatikanaji wa mikopo ili iweze kuwasaidia kuendesha miradi mbalimbali kama kununua mashine zinazotumia umeme za kufyatulia tofali, mashine za kukamua mafuta ya alizeti au mashine za kusaga na kukoboa hivyo amewaasa kutumia umeme kufanya shughuli za maendeleo ambazo zinakuza uchumi.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa