Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Ligunga amepongezwa kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa vyoo katika shule yake wakati kamati ya Fedha ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashuri Mhe. Menas Komba ikikagua miradi ya ujenzi wa vyoo vya shule za msingi Kata ya Kizuka na Muhukulu.
Ambapo pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha amemuomba kumaliza ukarabati wa Madarasa yaliyobaki wakati huo kamati ya Fedha ilichangia hapo hapo kiasi cha shilingi 90,000 kwaajili ya ukarabati wa milango ya Madarasa katika shule hiyo ambapo Mwenyekiti pia amemwambia kuna fedha ambazo zimetengwa na Serikali kwaajili ya kumaliza Madarasa yaliyobaki. Amesema
"Tumepita sehemu nyingi sana lakini hapa umefanya vizuri sana richa ya umbali wa mradi hakika unastahili pongezi nyingi kupitia ujenzi huu kwahakika umezitendea vema fedha za Serikali maana tumeona vyoo safi pia umejenga kinawia mikono kiasi kwamba inaonekana hamna ulaji wa hela katika mradi huu. Kwahiyo nikuombe tu kwa fedha hizi ambazo umechangiwa hapa malizia kukarabati milango ya madarasa ambayo haifungi vizuri ili kuweka taswira nzuri ya shule hii hata hivyo Serikali imeshatenga fedha kiasi cha shilingi milioni 12 kwaajili ya ukarabati wa madarasa( darasa la awali ) na ofisi iliyobaki"
"Pia niwaombe walimu wengi japo kwa uchache wenu lakini naombeni toeni ushirikiano kwa mwalimu Mkuu wenu na hata Serikali kwa kutulindia watoto wetu na kuwafundisha kwani Serikali inatoa fedha nyingi kwaajili ya watoto wetu wapate Elimu bora" Alisema Mhe Menas Komba Mwenyekiti wa Kamati.
Alitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Ligunga Madawa John Java amesema "Tulipokea kiasi cha shilingi 33,993,862.66 kwaajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo13 na iliyobaki ni shilingi 2,636, pia stoo tumebakiwa na sinki moja la kunawia mikono, marumaru, pipe ya maji na kopo moja la rangi"
Pia Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Ligunga ameahidi kukarabati milango ya madarasa kutokana na fedha alizochangiwa na kamati hiyo na kusema Hadi tarehe 24 ya mwezi huu Octoba atakuwa amekamilisha. Pia kamati hiyo iliendelea na ukaguzi katika shule nyingine kama vile shule ya Msingi Lizaboni, Shule ya Msingi Lunyere na kumalizia Shule ya Msingi Lung'oo Kata ya Muhukulu.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa