Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Afya. Mhe. Jenista Mhagama amezindua Vyumba 17 vya madarasa na vyoo Matundu 25, katika Shule ya Sekondari Mpitimbi, pamoja Vyumba 10 vya madarasa na matundu ya vyoo 19 katika Shule ya Sekondari Jenista Mhagama.
Katika ziara hiyo, Mhe. Jenista aliambatana na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Songea, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea pamoja na Timu ya Watalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Akisoma taarifa, Mkuu wa Shule ya Mpitimbi alisema “ Shule ilipokea kiasi cha Tshs 452,000,000/= kwa ajiri ya kujenga madarasa mapya 17, na Matundi 25 ya vyoo, ambapo hadi sasa mradi huo umekamilika kwa 100% na tayari wanafunzi wameanza kuyatumia
Aidha Mkuu wa Shule ya Sekondari Jenista Mhagama, alisema “Shule imepokea kias cha Tsh. 273,000,000/= kutoka Serikali kuu kwa ajili ya Ujenzi wa Madarasa 10, na Vyoo matundu 19 na yameanza kutumika
Mhe. Jenista amefanya uzinduzi huo jana Machi 16,2025 katika Kata ya Mpitimbi na Parangu, akiwa kwenye ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea ikiwa ni muendelezo wa ziara za kukagua Miradi ya maendelea katika Jimbo lake lakini pia kuzungumza na wananchi.
Akiwa kwenye Ziara hiyo, Mhe Mbunge alifikisha salam za Upendo kutoka kwa Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wa Songea, na kuwashukuru kwa heshima waliyompa ya kusaidiana nae katika kuleta Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa