Walengwa wa kaya masikini katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma wameshukuru mfuko wa TASAF kwa kusaidia kuwasomesha watoto.
Wakizungumza kwa nyakati taofauti mjini Madaba,wamesema wanashukuru mfuko wa TASAF kuwasaidia kusomesha watoto wao kuanzia ngazi ya awali hadi kidato cha nne,tofauti na awali ambapo walikuwa wakishindwa kumudu gharama za kuwanunulia watoto wao sare za shule,viatu na madaftari.
Chistina Lwambano,Patesta mkinga ni miongoni mwa wanufaika na mfuko wa TASAF kuanzia mwaka 2015, wamesema tangu waanze kuhudumiwa wamepata mafanikio makubwa pamoja na kujenga nyumba za bei nafuu ukilinganisha na makazi duni ambayo walikuwa wanaishi hapo awali pia uhakika wa upatikanaji wa chakula katika kipindi chote cha mwaka.
“Na kweli naishukuru TASAF imenitoa katika makazi maduni na kuniwezesha kujenga nyumba na kusomesha watoto wangu wanne’’,alisema Patesta Mkinga.
Aletruda Wella,Frivia Mbilinyi na Agnes Mgimba wamesema Mfuko wa TASAF, umewaondoa katika hali ya unyonge ambayo wlikuwa wakijiona wao sio bora katika jamii kuanzisha shughuli nyingine ndogondogo kama vile ufugaji wa kuku wa kienyeji,mbuzi na shughuli za kilimo.
Wanufaika hao wameiomba TASAFkuwasaidia pembejeo za kilimo wakati wamasika ili waweze kumudu gharama za kilimo na kupata mavuno mazuri
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa