Mbunge wa jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, ( Sera, Bunge na Uratibu) Mhe Jenista Joakim Mhagama, amezindua Mradi wa Maji wenye thamani ya Shilingi Milion mia sita kumi na nane (618,000,000/=) katika kata ya Litapwasi kijiji cha Lyangweni
“Leo Lyangweni tumemtua mama ndoo kichwani, maji yanapatikana,. Maji hayo tumekwenda kuchimba kisima kirefu ambacho kinauwezo kwa siku kuzalisha lita laki moja na sitini na nane lakini mahitaji yetu kwa siku hapa Lyangweni ni lita laki moja na hamsini na tisa, kwahiyo maji yanayozalishwa ni mengi kuliko yanahitajika kutumiwa nani kama Mama Samia?. Alisema Mbunge wa Jimba la Peramiho
Mradi huo wa Maji uliopo kijiji cha Lyangweni, unathamani ya Tsh. 618,000,000 unahudumia wananchi wapatao 2,159 wa kijiji cha Lyangwenina umetekelezwa kwa njia ya Force Account” na kwa sasa umekamilika kwa asilimia mia moja 100%.
Akizungumza kwa kwa niaba ya Meneja wa RUWASA, Eng. Hamisi Yasini amesema “ Mhe. Mbunge, hadi sasa mradi umetekelezwa kwa asilimia 100 kwa maana mradi huu umekamilika na unatoa huduma kwa wanachi.
Aidha Eng. Yasini ametoa Faida za Mradi huu kwa wananchi wa Lyangweni ikiwemo, kupunguza umbali mrefu wa wananchi kwenda kutafuta maji, Kupunguza athari za kupata Mlipuko wa magonjwa kwa kukosa maji safi na Salama.
Hata Hivyo Mhe. Jenista Mhagama aliwasihi wananchi wa kijiji cha Lyangweni kutunza miundombinu ya mradi huo wa maji ili kufanya mradi huo uwe endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa