Waziri Ofisi ya waziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira Kazi Vijana na walemavu na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista hagama amekabidhi bomba za kusambazia maji zaidi ya 300 zenye thamani ya Tsh.milioni 56 kwa Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini Songea kwalengo la kujenga na kuboresha miundo mbinu ya huduma ya maji katika Kijiji cha Mbingamharule Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.
Mhe,mhagama amekabidhi bomba hizo kufuatia tatizo la upungufu wa upatikanaji wa huduma ya maji Kijijnii hapo baada ya mabomba ya awali ambayo yalikuwa yakisafirisha maji kutoka kwenye chanzo cha Mto Lilua hadi kwenye tanki kuchakaa.
Kuchakaa kwa bomba hizo kumesababisha adha kwa wananchi kupata maji kwakiasi kidogo ukilinganisha na mahitaji yao halisi kwa siku.
Mhe.Mhagama ametoa wito kwa wananchi wa Kijiji hicho kuunganisha nguvu zao kuchimba mtaro umbali wa kilomita nne utakao tumika kulaza bomba za kusambazia maji toka kwenye chanzo hadi kwenye tanki.
Kwa upande wake Meneja wa RUWASA wa Songea Mathias Pakras amesema bado kunatatizo kubwa la wananchi kuharibu vyanzo vya maji kwa kufanya kazi za kibinadamu ambazo zinasababisha vyanzo kuharibika na ufanisi wa vyanzo kuwa mdogo.
Pakras amezitaja hatua ya ujenzi wa mradi kuwa umefikia asilimia 65 na kazi mbalimbali zilizofanyika ni pamoja kujenga tanki lenye ujazo wa lita 75000,ukarabati wa vituo vya kutolea maji 33 na ukarabati wa bomba za usambazaji maji kwenye sehemu zenye mivujo ya maji.
Amezitaja kazi zilizo salia ili kukamilisha mradi kuwa ni ukarabati wa vituo vya kuchotea maji na mivujo kwenye bomba za usambazaji maji.
Naye Diwani wa kata hiyo Mhe,Nasri Mseremy Nyoni ametoa shukrani kwa Mbunge na Uongozi wa Halmashauri kwa kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya ,hosteli kwa ajili ya wasichana katika shule ya sekondari Mharule, nyumba za ibada na miundo mbinu ya barabara ,kitendo kinachojenga Imani baina ya wananchi na Serikali yao.
Amewarai wananchi wake kujenga mshikamo na ushirikano wanapohitajika kutekeleza majuku mbalimbali ya kijamii na ya Serikali kwa lengo la kupata mabadiliko chanya ya maendeleo.
Imeandaliwa na
Jacquelen Clavery
A/habari Songea DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa