MBEGU ZA MUHOGO
Wakulima wa Halmashauri ya Wilaya yaSongea wamehizwa kuchangamkia fursa ya kupanda mbegu ya muhogo au vipando kwa lengo la kupata mbegu ya msingi zitakazozalisha zao muhogo
Hayo yamesemwa na BI HELENI KIOZYA kutoka Taasisi ya Utafiti wa mazao ya Mizizi Kibaha Mkoani Pwani na BI LINDA MALULI kutoka shirika lisililokuwa la kiserikali la MEDA(Menonite Ecomic Development Association) katika mafunzo elekezi ya kuwatambua wakulima watakaokidhi vigezo vya kupanda mbegu ya zao muhogo kwa Waheshimiwa madiwani na wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hivi karibuni.
Bi Kiozya amewahimiza wakulima kuchangamkia fursa kupanda mbegu za zao la mihogo kama moja ya zao la biashara ambalo litasaidia kuinua uchumi wao kutokana na viwanda vya kusindika mihogo kuhitaji mihogo kusindika na kuzalisha bidhaa mbalimbali licha ya kuzalisha kama zao la chakula.
Amesema baada ya kuwatambua wakulima watakao panda mbegu za zao la mhogo kila mkulima atatakiwa kuwa na ekari 4 kwa kuanzia,ambapo kila ekari moja atapanda mbegu 4000 baada ya kukuza mkulima atauza kila mbegu moja shilingi 200 kwa watakao hitaji mbegu,na baada ya miaka mitatu mkulima ataanza kuvuna mihogo tayari kwa chakula.
Mahali au sehemu inayotakiwa kulimwa na kupanda mbegu ya zao la muhogo haitakiwa kuwa karibu na mashamba mengine ya zao la muhogo kwa lengo la kuepuka magonjwa yanayoshambulia mihogo kama vile bato bato na kumsababishia hasara mkulima
Mbegu zitakazo tolewa kwa wakulima nizile zilizo fanyiwa utafiti na Taasisi za Serikali kutoka Naliendelee Mkoani Mtwara,Kibaha Mkoani Pwani na Uyole Mkoani Mbeya na mbegu ambazo zimethibika kuwa na ubora ni aina ya kiroba,Mkuranga, kizimbani,Chereko na Kipusa ambazo hustamili magonjwa ya mihigo.
Zao la mhogo hustawi vizuri Zaidi katika kata zote 16 za Halmaashaauri ya Wilaya ya Songea kufuatia hali ya hewa mchanganyiko
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa