Marufuku wananchi kuanzisha shule shikizi kiholela
Agizo hilo limetollewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh Christine Mndeme kakika kikao maalumu cha baraza la madiwani kilicho fanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Mh Mndeme amesema marufuku wananchi kuanzisha shule shikizi kiholela kwasababu zimekuwa zikianzishwa bila utaratibu unaotakiwa kufuatwa na kusabisha adha ya ukamisha wa shule hizo kwakuwa srikali inatekeleza mipango yake kulingana na bajeti.
Mndeme amewataka madiwani kusimamia na kuhakikisha shule shikzi hazianzishwi kiholela na pasipo sababu yoyote msingi na endapo itatakiwa huduma ya shule utatakiwa ufuatwe utaratibu wa kujenga shule na sio shule shikizi,na diwani atakae husika na swala hilo jukukumu la kukamilisha ujenzi na utoaji wa huduma litakuwa juu yake.
Shule shikizi zimekuwa zikianzishwa kufuatia wananchi kuhama makazi yao awali na kuhamia mashambani kwa lengo la kutafuta maeneo ya kulima jambolo ambalo ni gumu kufikiwa na huduma za kijamii kwa wakati badala yake waanzishe makazi ya kudumu sambamba na ujenzi wa vyumba bora ambazo zitasaidia kuondoa tatizo la kuhama hama na kupatiwa huduma za jamii kwa urahisi.
Halmashauri ya Wilaya ya Songea ina shule shikizi nane ambazo ni Lunyele,Jenista, Selekano,Mbolongo,mingine ni Luhuhu,Ulamboni Maleta na Mwimbasi huku shule za msingi zikiwa 69.
Ameongeza kwakusema miradi yote iliyo ibuliwa na wananchi,Halmashauri iunge mkono nguvu za wananchi hao kwakuyakamilisha na yaanze kutoa huduma wanazozihitaji,kwakuwa miradi ya maendeleo hutoa fursa za kiuchumi kwa wananchi
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa