Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songea imefanya Ziara ya siku mbili ya kukagua miradi inayoendelea katika Halmashauri.
Ziara hiyo ya siku mbili kuanzia tarehe 15-16/01/2024 imekagua miradi ya maendeleo ambayo ni
Magwamila shule ya msingi Jenista shule ya msingi, Mbiro shule ya msingi, Ulamboni shule ya msingi na Magagura Sekondari
Akizungumzika katika Ziara hiyo, Mhe. Simon Kapinga, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri, alisema lengo la ziara hiyo ni kuatilia utendaji na maendeleo ya miradi, lakini pia kusisitiza na kuweka nguvu pale ambapo hapaendi sawa.
“ Hiki ni kipindi cha Mvua, tunahitaj kasi kwenye miradi ili kuhakikisha tunaendana na hali ya hewa ya sasa. Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya kukamilisha miradi, hivyo ni jukumu letu kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati.
Aidha amepongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluh Hassan kwa namna inavyowekeza nguvu katika kutatua kero na changamoto za wananchi.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa