Afisa Mwandikishaji Jimbo la Peramiho, Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Bi. Elizabeth Gumbo, April 29,2025 amefungua mafunzo ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Mafunzo hayo ya siku moja, yamefanyika katika Ukumbi wa Jenista Mhagama uliopo Shule ya Sekondari Maposeni
" Nimatumain yangu kuwa , kutokana na Semina hii, kila mmoja wenu atapata elimu ya kutosha itakayomwezesha kutekeleza majuku yake ili kufanikisha zoezi hili" Gumbo
Mafunzo hayo, yatahusisha namna bora ya ujazaji wa Fomu, Kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura ( Voters Registration System) Pamoja na Matumizi sahihi ya vifaa vya uandikishaji wa wapiga kura.
Aidha katika mafunzo hayo, aliwaapisha Maafisa waandishaji wasaidizi Kiapo cha kutunza Siri na Tamko la kujitoa Uanachama au kutokua mwanachama wa Chama cha Siasa, Lengo ikiwa ni kuhakikisha zoezi hili linaenda bila ya kuwa na mgongano wa kimaslahi.
Gumbo ameweka wazi kuwa Mawakala wa Vyama vya Siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura, akisema kuwa wamefanya hivyo ili kuweka uwazi katika zoezi zima lakini pia mawakala hao watatumika kutambua wapiga kura wa eneo husika.
Wito ulitolewa kwa Maafisa hao kuweka ushirikiano mkubwa kati ya watendaji wote wa uboreshaji, Serikali, vyama vya Siasa na wadai wengine wote wa Uchaguzi
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa