Mafunzo elekezi ya usimamizi wa uchaguzi
Wasimamizi wa uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Peramiho wametakiwa kufuata sheria kanuni na taratibu za uchaguzi
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bw Simoni Bulenganija wakati akifungua mafunzo kwa Washiriki wa mafunzo ya usimamizi wa uchaguzi mdogo wa udiwani katika jimbo la Peramiho kata ya peramiho mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Emau Peramiho hivi karibuni .
Bw Bulenganija amesema wasimamizi wazingatie sheria,kanuni na taratibu zinazotakiwa ilikufanikisha kazi ya uchaguzi na kwa uweledi mkubwa.
Amesema swala la uchaguzi ni swala nyeti ni vema wawemakini na kazi yao na kujaza fomu zinazotakiwa kwa usahihi
Akizungumza kwa niaba ya wengine moja ya wasimamizi hao Bw Zakaria Kapinga amesema watazingatia maelekezo yote na kuhakikisha kazi ya uchaguzi inafanyika kwa ufanisi.
Jumla ya wasimamizi 57 wamepatiwa mafunzo elekezi ya usimamizi wa uchaguzi na vituo 19 vya kupigia kura.
Jacquelen clavery_TEHAMA
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa