Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Kupitia Divisheni ya Maendeleo ya Jamii wameanza mchakato wa Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi.
Siku ya wanawake duniani, (8 Mach) hutumika kuwaunganisha wanawake wote duniani kujadili maswala mbalimbali kuhusu maswala yanayowahusu lakini pia kukutana pamoja kwa lengo la kusaidia jamii kwa mambo yanayowazunguka ikiwa ni pamoja na matendo ya Huruma.
Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Kupitia Divisheni ya Maendeleo ya Jamii kama ilivyo kwa Halmashauri nyingine wamejipanga kuadhimisha siku hiyo kwa kufata maelekezo kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum ambapo pamoja na mambo mengine wamegawanyisha majukumu kwa kila siku kabla ya kufika tarehe 8 Marchi 2024.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Bi. Sophia Ndibahezwa amesema “ maandalizi ya siku ya wanawake duniani ambayo yataanza tarehe 1.03.2024 mpaka 8.03.2024, ambapo tarehe 1 machi tutakua na amsha hari ambapo kamati ya maandalizi itashirikiana na wananchi wa kata ya Liganga kufanya usafi kwenye ujenzi wa chuo cha walemavu kilichopo kwenye kata hiyo.
02.03.2024 Tutaenda kufanya matendo ya huruma kama inavyoelekeza Wizara, matendo hayo yatahusisha kutoa mahitaji kwa watu wenye mahitaji maalumu, lakini pia tutaenda kutoa chakula mavazi kwa watu walioathiliwa na ukoma. Sambaba na hili tarehe 04.03.2024 kutakua na kongamano la wanawake, ambapo wanawake kutoka sehemu tofauti watapata elimu ya Ujasiliamali, elimu ya fedha, elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia, sheria za mirathi na umiliki wa mali, kizazi chenye usawa lakini pia elimu ya makuzi na malezi ya watoto kwa ajili ya ustawi wa familia zetu.
Aidha tarehe 06.03.2024 tutafanya uzinduzi wa siku ya wanawake katika Halmashauri ya Wilaya ya songea tutayafanya katika kata ya Liganga ambapo wananchi wote watashiriki. Maadhimisho haya kwa mwaka 2024 yanaongozwa na kauli mbiu “ Wekeza kwa Wanawake kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii”. Kauli mbiu hii inalenga kuhamasisha Jamii kuwekeza kwa Wanawake ili kuleta Usawa wa Kijinsia pamoja na kukumbushana umuhimu wa usawa wa kijinsia katika kuchochea ukuaji wa Uchumi, Maendeleo Jumuishi na Ustawi wa Jamii kwa Maendeleo endelevu kwa Wanawake.
Hivyo siku ya kilele ambapo ni tarehe 08.03.2024, wanawake wote kutoka Wilaya zote Mkoa wa Ruvuma tutakutana Wilaya ya Mbinga kwa ajili ya Kuadhimisha siku hiyo.
Divisheni ya Maendeleo ya jamii imepongeza na kushukuru mchango uliotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mwl. Neema Maghembe kwa kufanikisha shughuli hiyo.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa