WILAYA ya Songea imefanya maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Maadhimisho hayo yaliudhuriwa na Viongozi, Taasisi mbalimbali, watumishi wa Halmashauri za Wilaya ya Songea na Wageni kutoka Zanzibar.
Akizungumza Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Kamando Mgema ambae amewakilishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mheshimiwa Michael Mbano amewahasa Wananchi kila mmoja kwa nafasi yake aweze kulinda Uhuru wake kwani ni jukumu la kila mtu.
‘’ Ndugu zangu tumekutana hapa ili tuweze kufanya tafakari, tafakari ambayo itatuonyesha wapi tumetoka, wapi tulipo na tunatamani twende wapi’’, amesisitiza Mheshimiwa Mbano.
Aidha, Mheshimiwa Mbano amesema Uhuru unalindwa kwa kufanya kazi hivyo matatizo yanayowapata Watanzania yanapaswa kutatuliwa na Watanzania wenyewe hata hivyo ameongeza Watanzania wahimizane kwenye swala zima la Uzalendo kwaajili ya maendeleo ya Taifa.
Kwaupande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Ndugu Pendo Daniel ameelezea maudhui ya maadhimisho hayo amesema Nchi ya Tanzania ilikua ni koroni la Waingereza hivyo tarehe 9 Desemba 1961 ndipo Uhuru ulipatikana.
‘’Hivyo kabla ya Uhuru Waingereza waliifanya Tanganyika kama sehemu ya kupata Malighafi lakini hakuweka miundombinu ya kutosha na miundombinu michache waliyoiweka ilikua kwa lengo la kuwasaidia wao kusafirisha malighafi hizo’’, amesema Ndugu Pendo.
Ndugu Pendo ameongeza kuwa maadhimisho hayo yamelenga kuwajengea wananchi wa Wilaya ya Songea Uzalendo ili kujua nini Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanya kwa miaka 61 ya Uhuru.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa