Lishe ni kichocheo cha maendeleo kufikia uchumi wa kati wa viwanda hivyo swala la lishe katika jamii liwekewe mkazo ilikuepuka madhara makubwa yatokanayo na ukosefu wa lishe ambayo ni udumavu unaopelekea kuathiri uchumi wa familia na Taifa
Hayo ameyasema Mkuu wa wilaya ya Songea Pololeti Mgema wakati akifungua kikao cha lishe kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Songea.
Mhe Mgema amesema swala la lishe nikichocheo cha maendeleo hivyo litiliwe mkazo kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa lengo kuepuka madhara makubwa yatokanayo na ukosefu wa lishe ambayo ni udumavu ,ulemavu kama vile upofu,na kusababisha vifo.
Fatma Mwasola ambaye ni Afisa Lishe Mtafiti kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) amesema Tanzania inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wototo wenye udumavu kwa asilimia 31.8 nakujifungua watoto chini ya uzito pungufu wa kilo2.5 unaosababishwa na lishe duni ,mazingira machafu kama vile vyoo,mgawanyo mbaya wa rasilimali na mila potofu.
Mwasora amesema ni vema wadau mbalimbali wa lishe wakafanya lishe ni agenda ya maendeleoo katika jamii na Taifa kwasababu ya kuokoa vifo vya watoto, kina mamawajawazito,kuokoa fedha ambazo Serikali inagharamia kununua vifaa tiba na dawa kama vile chakula Lishe, jamii kutumia muda mwingi kuhudumia wagonjwa badala ya kufanya shughuli za kiuchumi ambazo zitatupelekea kufikia uchumi wa kati wa viwanda.
Ameongeza kwa kusema udumavu huanzia tumboni kwasababu mbalimbali kamavile ukosefu wa kingamwili,lishe duni,ukosefu wa makundi mchanganyiko ya vyakula sababu nyingine ni wajawazito kutomeza dawa za kuongeza damu kwa wakati na madini ya kalishamu pamoja na madini joto.
Matumizi ya chumvi hasa yamawe ambayo haina madini joto ni hatari kwasababu ni chanzo kikubwa cha udumavu,kuzaa moto njiti,uzito pungufu chini ya kilo 2.5, na watoto wenye mtindio wa ubongo.
“Tuwekeze katika lishe kufikia dira ya maendeleo kufikia uchumi wakati”alisema Mwasora.
Aidha Mkoa wa Ruvuma unaasilimia 41 yatatizo la udumavu na tatizo la kujifungua watoto chini ya kilo 2.5 asilimia 11 tatizo ambalo linatakiwa kuwekewa mikakati ya kulipunguza au kulimaliza.
JACQUELEN CLAVERY-AFISA HABARI
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa