Kuitwa kaya masikini basi baada ya kusaidiwa na TASAF
Hayo yamesemwa na baadhi ya walengwa wanao nufaika na mfuko wa kunusuru ka masikini nchini TASAF wakati walipotembelewa na mratibu wa wa mfuko wa kunusuru kaya masiki wa halmashauri ya wilaya songea mkoani Ruvuma hivi karibuni.
Yosefa Honde na Agnela Magimba ni miongoni mwa walengwa wanaonufaika na mfuko wa TASAF wanasema kw nyakati tofauti wao sio kaya masikini ukilinganisha na changaoto za maisha walizopitia ukilinganisha na maisha yao wanayoishi sasa.
“Tangu nizaliwa mwaka 1963 sijawahi kulala nyumba ya bati ila kwa msaada wa TASAF nalala nyumba ya bati,”alisema bibi Yosefa Honde mkazi wa kijiji cha matimira kata ya Matimira katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Amesema tangu aingizwe kwenye mpango mwaka 2015 amekuwa akiweka akiba kidogo kidogo hatimaye fedha hizo zimemwezesha kujenga nyumba ya bati na kuanzisha shamba la matunda lenye ukubwa wa hekali mbili na matunda hayo amesha anza kuuza sokoni nakujipatia kipato ambacho kinamwezesha kujikimu kimaisha pamoja na familia yake.
Matunda aliyolima ni matango,malimau, machungwa, machenza na ufugaji wa kuku wakienyeji.Pia anatoa wito kwa walengwa wanzake kuiheshimu pesa wanayosaidiwa kwakuanzisha miradi midogo midogo ambayo itawasaidia kupunguza umasikini wa kipato katika familia zao.
Agnela Mgimba ni mkazi wa Halmashauri ya Madama ametelekekezwa na mume wake zaidi ya miaka 8,baada yakutelekezwa alipata changamoto kubwa ya kuwalea watoto wake watano kwa kuwapa mahitaji yote ya msingi yakiwemo chakula ,mavazi na malazi.
Mara baada ya kuingizwa kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini mwaka 2015 kutokana kiasi cha fedha anachopata ameweza kujenga nyumba ya tofari na kupaua bati kuanzisha shamba la mbogamboga na matunda pamoja na mradi wa kufuga kuku wakienyeji na nguruwe ambayo yanauwezesha kumudu gharama za maisha na kuwasomesha watoto wake ambao wanasoma sekondari.
Anasema haelewi mume wake alipo anachoweza kusema ni asante kwa serikali kwakuwasaidi kupitia TASAFU na endapo mradi TASAF utakwisha anauwezo wa kumudu changamoto za maisha.
JACQUELEN CLAVERY –TEHAMA-HABARI
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa