Kituo cha Afya Muhukuru Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma cha anza kutoa huduma za upasuaji kwa wagonjwa
Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Dkt Geofrey Kihaule ameyasema hayo wakati akizundua rasmi zoezi la upasuaji lililofanyika hivi karibuni kituoni hapo.
Amesema huduma za upasuaji zimeanza rasmi Kituoni hapo hivyo wananchi wenye matatizo ya upasuaji wafike katika kituo hicho kwa ajili ya kupata haduma badala ya kusumbuka kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 100 kufuata huduma hizo katika Hositali ya Mkoa na Peramiho
Dkt Kihaule amewataka wananchi kuondoa hofu kuhusu huduma hiyo kwasababu tayari madaktari na vifaa tiba vipo, changomoto ni upungufu wa vitanda kwasababu za kijiografia ya Tarafa ya Muhukuru wanatarajia kupata wagonjwa wengi wenye uhitaji kuliko vitanda vilivyopo vya kuwalaza wagonjwa.
Ameyataja magonjwa ambayo yanayofanyiwa upasuaji nipamoja na akinamama wajawazito wenye matatizo ya uzazi,ngiri mabusha na magonjwa mengine yanohitaji upasuaji.
Amesema tayari wamefanikiwa kupasua wagonjwa watatu wa mabusha ambao walikuwa wkisumbuliwa kwa muda mrefu na mama mmoja mjamzito aliyekuwa na matatizo ya uzazi.
Baadhi ya wananchi wameishiukuru Serikali ya awamu ya tano kwa hatua ya kuboresha Vituo vya kutolea huduma ya Afya ikiwa ni pamoja na kuanzisha rasmi huduma ya upasuaji kwa akina mama wajawazito na magonjwa mengine katika kituo cha Afya cha Mhukuru.
Wananchi hao wamesema kuwa kabla ya huduma hiyo kuanza kutolewa walikuwa wanalazimika kutembea umbali zaidi ya kilomita 100 kwenda Hosptitali ya Rufaa ya Mkoa kufuata huduma ya upasuaji jambo ambalo limesababisha baadhi ya wagonjwa kupoteza maisha kabla ya kupatiwa huduma, huku Halmashauri ikiingia gharama kubwa kusafirisha wagonjwa.
Naye Diwani wa kata ya Mhukuru Lilahi Simon Kapinga amesema kuwa uwepo wa huduma hiyo utasaidia kupunguza vifo kwa akina mama wajawazito wenye uzazi pingamizi pamoja na watoto wadogo ambao ndiyo wahanga wakubwa na kupunguza gharama kwa serikali na wagonjwa.
Kapinga amesema kutokana na ubovu wa barabara gari la wagonjwa wakati mwingine lilishindwa kumfikisha mgonjwa Hospitali kwa wakati hivyo hatari ya kifo ilitawala zaidi kwa sasa wagonjwa wengi watahudumiwa kwenye kituo chao kwa wakati.
Halmshauri ya Wilaya ya Songea ina jumla ya vituo vya Afya vitano,Hospitali ya Wilaya moja ambayo haijaanza kutoa huduma hata hivyo wilaya hiyo kuna Hospitali ya Misheni ya Peramiho ambayo wananchi wengi wanatumia Hospitali hiyo kupata huduma ya Afya kama Hospitali ya Rufaa.
JACQUELEN CLAVERY
AFISA HABARI
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa