Kikao cha Tathmin ya Elimu Halmashauri ya Wilaya ya Songea, kilichofanyika tarehe 4/12/2024 katika ukumbi wa Jenista Mgahama kimesisitiza Walimu kujituma zaid katika kutimiza majukum yao
Kikao hicho kilichoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe. Kapenjama Ndile, ambapo pamoja naye, alikuwepo pia Kaimu Afisa Elimu Mkoa, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Maafiisa Elimu kata, Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari.
lengo la kikao hicho ni kujitathmini baada ya kutoka kwa matokeo ya Darasa la Saba, ili kuangalia wapi wameanguka na wapoi wapo imara ili kujiweka sawa kwa ajili ya mwaka ujao.
“ Tumeamua kufanya tathmini ya matokeo tuliyonayo mkononi na kuangalia miaka miwili iliyopita ili kujitathmini kuona wap tunafanya vizur na wapi hatufanyi vizuri na njia gani zitumike kwa mwaka ujao” Elizabeth Gumbo, Mkurugenzi Songea Dc
Mkuu wa Wilaya ya Songea pamoja na mambo mengine, aliwataka walimu kuhakikisha sio tu wanazingatia ufaulu, lakini pia wajikite katika kumsaidia mwanafunzi kupata ujuzi ambao utamsaidia kubadili maisha anayoishi.
“ Lengo kubwa la Elimu si tu kufaulu mitihani, bali lengo ni kumfanya mwanadamu abadili maisha anayoishi ili yawe mazingira rafiki zaidi kwa kuishi”
Hata hivyo walimu walikumbushwa kutokufanya shughuli binafsi kwenye muda wa kazi, kuheshimu kazi yao na kuhakikisha wanatengeneza mazingira rafiki kati yao na wanafunzi ili kurahisisha uelew kwa wananfunzi
“ Wapo baadhi ya Walimu hutumia muda wa kazi kufanya shughuli zao, na wengi wamekua wakienda shamba muda wa kazi, huu ni utoro na kama tutaundekeza tutashindwa kufikia malengo yetu kwa ajili ya walimu wachache, hilo pia hatutolikubali”
Tathmini ya Elimu imekua ikifanyika mala kwa mala lebgo ikiwa ni kujitathmini na kuendelea kuweka nguvu kwenye mapungufu yanayojitokeza.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa