Mfuko wa kuhudumia kaya maskini nchini katika Halmashauri ya wilaya ya songea Mkoani Ruvuma umeanza utaratibu wa kuwalipa fedha walengwa wa kaya maskini kwa njia ya kidigitali huku baadhi ya walengwa wa mfuko huo wakilalamikia changangamoto ya ukosefu wa mawasiliano ya mtandao wa simu na baadhi yao kutojua kabisa matumizi ya simu.
Mratibu wa TASAF wa Halmashauri hiyo Hossana Ngunge amesema utaratibu huo umeanza kutumika mwezi Julai 2021 na kuendelea hivyo walengwa wote wanatakiwa kujisajili kwenye mitandao ya simu ambayo wataitumia kupokelea fedha zao.
Ngunge ametoa ushauri kwa makampuni ya simu kutumia fursa ya kwenda katika maeneo ambayo bado hayana mawasiliano ya simu na yenye mawasiliano yasiyokuwa na uhakika kuyafikia maeneo hayo ili walengwa wa kaya maskini na wananchi wengine waweze kunufaika na huduma hizo.
Ameongeza kwakusema utaratibu wa kuwalipa kaya maskini kwa njia ya simu kutasaidia kuondoa changamoto ya gharama za zoezi la kuwafikishia walengwa fedha zao na baadhi ya walengwa kudhulumiwa na watu wasio waaminifu ambao waliokuwa wakiwatuma kuwachukulia faedha hizo.
Kwa upande wao baadhi ya walengwa wa kaya maskini wameulalamikia utaratibu wa kupokea fedha kwa njia ya simu kwao umekuwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na wao kutokuwa na uelewa juu ya matumizi sahihi ya simu hivyo kupelekea fedha zao kuporwa na wategemezi wao bila wao kutambua na kuomba wapatiwe fedha zao kwa njia ya tasilimu.
Halmashauri ya Wilaya ya Songea ina jumla ya kaya masikini 6,143 kati ya kaya hizo 3,731 ziliingizwa kwenye mpango tangu awamu ya kwanza kutoka Vijijiji 32 na awamu ya pili kaya 2,412 zimeingizwa kwenye mpango wa kupima matokeao ya kunusuru kaya masikini kwenye vijiji 24 na wataanza kulipwa baada ya kufanyiwa tathimini.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa Habari
Songea DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa